MATATIZO SUGU YA KOMPYUTA ,MBINU ZA KUONDOA TATIZO


Ni siku nyingine ambapo tunakutana kwenye Ukurasa huu, hili tupate kujifunza yale matatizo yanayoikumba Kompyuta yako pamoja na mbinu au suluhisho la tatizo hilo. Kwa leo tutazungumzia tatizo liflifuatal                
1. KOMPYUTA KUWA NZITO. (COMPUTER TO WORK SLOWLY/STUCKING).

Hili limekuwa tatizo ambalo husababisha utendaji wa kazi wa Kompyuta yako kuwa mdogo au kuwa nzito sana na hata kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Yafuatayo ni mataizo/sababu kuu Duniani ambazo mpaka sasa yanafanya Kompyuta nyingi kuwa nzito(SLOWLY).

(i) VIRUSI(VIRUSES)
Virus ni “software” ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuharibu “software” nyingine ambazo zinakuwa kwenye mfumo wa utendaji wa Kompyuta.
Yafuatayo ni madhara yasababishwayo na Virusi kwenye Kompyuta.
(a) Kupotea kwa files/ taarifa kwenye Kompyuta., hapa kirusi kikishaingilia file kina uwezo wa kulifuta, kuficha, kutafuna au kuliondoa kabisa kwenye Kompyuta.
(b) Kuharibu mfumo wa Utendaji wa Kompyuta (Operating System corrupt). Hapa hutokea kwa sababu hivi virusi vinakuwa na nguvu kubwa kuliko mfumo wa utendaji wa Kompyuta. (Operating System).
(c) Kompyuta kuwa nzito sana(slowly) ambapo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa sababu mfumo mzima wa utendaji unakuwa umelemewa na virusi.
(ii)HARD DRIVE DISK (HDD).
HDD ni kifaa ambacho hutunza taarifa, ambacho ni “hardware”, kwenye Kompyuta. Ndani ya HDD kuna kitu kinaitwa “Sector” ambacho ndicho kinachoendesha mfumo mzima wa utendaji kwenye Hard Disk, hivyo ikitokea mfumo mbaya wa utendaji wa “sector” (bad sector), hupelekea HDD kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi na hiyo hupelekea mfumo wa Utendaji wa Kompyuta (Operating System) kuwa nzito.
(ii) RANDOM ACCESS MEMMORY. (RAM)
RAM ni kichocheo muhimu sana katika utendaji mzima wa Kompyuta, mara nyingi hufanya kazi kama kibarua kwenye mfumo wa utendaji wa vifaa vitatu vinavyotegemeana hapa nina maana ya “RAM” yenyewe, “Processor” pamoja na “Hard Disk”. Na kazi kubwa ya RAM ni kutoa taarifa toka kwenye Hard Disk kwenda kwenye Processor, hicvyo kama RAM ina ukubwa mdogo hupelekea spidi kupungua na mwishowe Kompyuta kuwa nzito(slowly).

(iii) Kuchemka kwa “Processor”, hii hutokea pale ambapo mtu hana mazoea ya kufanya “service” kwenye Kompyuta yake, kitendo ambacho husababisha “Cooling system” kupata joto mwishowe husababisha Kompyuta kuwa nzito.
JINSI YA KUTATUA TATIZO LA KOMPYUTA KUWA NZITO.
1. Kuweka “Antivirus” kwenye Kompyuta yako, zipo aina mbalimbali za Antivirus kama eScan, Kaspersky, Adware, MacAfee, AVG n.k. Zipo Antivirus za kununua ambazo zinakuwa na uwezo mkubwa sana, pia zipo za kupakua(download) kwenye mtandao. Hapa tunapendekeza ununue ili kuwa na Ulinzi Imara wa Kompyuta yako.
2. Pia ni vyema kuwa na RAM yenye uwezo mkubwa ili kutokana na kazi zako jinsi zilivyo kwa ujumla.
3. Tunashauri kuwa na mazoea ya kufanya “SERVICE” kila mara ili kuifanya Kompyuta yako kuwa katika hali nzuri, pia yafaa ukawa na mazoea ya kuisafisha Kompyuta yako ili kuepuka vumbi kuingia kwenye Kompyuta yako, pia uonapo Kompyuta yako imeanza kuwa nzito wakati unaendelea kufanya kazi waweza pia “ku reboot” hapa nina maana ya “restart” na hata waweza “ku boot” ikiwa na maana ya “Start.”.

Somo hili la, “Matatizo yanayoikumba Kompyuta yako na Suluhisho lake” litaendelea, Endelea kutufuatilia…………
Karibuni sana kwa maoni na Ushauri, pia uwapo na tatizo lolote la Kompyuta usisite kututafuta.....ONE LOVE ™™™™™
™©

Comments

  1. Ahsante kwa elimu nzuri sana! Kuna mambo mengi nimejifunza na nitafanyia kazi!

    Elimu kuhusu kompyuta ni muhimu kwetu kwa sababu maisha ya sasa yanategemea sana kompyuta.

    Kutojua tatizo la kompyuta kutapelekea kutojua njia ya kulitatua.

    Tunashukuru blogu hii kwa kujaribu kuweka bayana matatizo ambayo tunaweza kuyatatua sisi wenyewe!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana kwa kutembelea .......usikose ndg yangu masomo yatakayofuata ....of course dunia ya leo pia inaenda kisasa

      Delete
  2. Dr Mvanda asante kwa elimu ambayo unatufungua macho

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI

VYAKULA NA MATUNDA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME