SHERIA 17 ZA MPIRA WA MIGUU
ZIFAHAMU SHERIA 17 ZA MPIRA WA MIGUU . 1. UWANJA Kwa kawaida uwanja wa mpira Wa miguu huwa na Urefu Wa mita 100 - 120 na Upana Wa mita 50 - 60 . Kwa kawaida Uwanja Wa mpira Wa miguu Una alama za mistari ambazo ni pamoja na - Mstari mrefu pembeni mwa Uwanja Unaoashiria mwisho Wa Uwanja . - Mstari mrefu Wa Katikati Unaogawa Uwanja katika pande 2 Zilizolingana .katikati ya Uwanja kuna mduara wenye nusu kipenyo cha mita 9.15. - Mstari mrefu Upande Wa goli Unaoashiria mwisho Wa Uwanja upande Wa goli . - Pia kuna nusu duara katika makutania ya Mstari Wa pembeni na Mstari Wa goli ambapo huitwa Kona . 2. MPIRA Mpira Wa miguu unaweza kutengenezwa kwa kutumia Ngozi , plastiki , au makunzi mengine yanayofaa . Kwa kawaida mpira Wa miguu huwa na kipenyo cha sm 68 - 70 na Uzito Wa gramu 410 - 450 na Ujazo Wa 1.1 - 1.6 . - Utofauti Wa Kipenyo na Uzito Wa mpira Wa miguu hutegemea Uwezo ama rika la mchezaji au watumiaji . 3. IDADI YA WACHEZAJI Mpira Wa miguu huchezwa na wachezaji 22...