BADO KAMUSOKO TU

Yanga imeanza kujifua wiki iliyopita ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa VPL pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23 dhidi ya Simba. Jumla ya wachezaji 16 wako kikosini wakiendelea na mazoezi. Lakini bado kiungo fundi Thabani Kamusoko hajarejea kutoka Zimbwabwe. Mkataba wa kiungo huyo umemalizika na tayari uongozi umeshamalizana nae juu ya kusaini mkataba mpya. Imeelezwa wakati wowote atatua jijini Dar es salaam kusaini mkataba mpya. Wachezaji ambao wako kambini wakiendelea na mazoezi ni wapya wanne; kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC. Wengine ni mabeki, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’. Viungo Geoffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Said Juma Makapu, Emmanuel Martin, Yussuf Mhilu, Obrey Chirwa na mshambuliaji Amissi Tambwe. Pia wamo Henry Okoh kutoka Nigeria na Fernando Bongnyang kutoka Cameroon ambao wanafanya majaribio. Wachezaji ambao hawapo ni pamoja na majeruhi wawili, kipa Benno Kakolanya na kiungo Deus Kaseke; mshambuliaji Donald Ngoma amesharejea na ataanza mazoezi wakati wowote. Beki Hassan Kessy na winga Simon Msuva wapo na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho leo Jumatano kinakwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda mwishoni mwa wiki kuwania tiketi ya CHAN 2018 nchini Kenya. Aidha Winga Simon Msuva hatakuwepo kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya kusajiliwa na klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI

VYAKULA NA MATUNDA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

MATATIZO SUGU YA KOMPYUTA ,MBINU ZA KUONDOA TATIZO