Karibu tena kwenye Ukurasa wetu huu ambapo tunaendelea kueleza matatizo yanayozikumba Kompyuta mbalimbali pamoja na suluhisho/mbinu za kuweza kutatua tatizo hilo. Tufuatane pamoja kutambua matatizo hayo ili tuwe na uelewa Zaidi.
-
1.KIOO KILICHOVUNJIKA/BROKEN SCREEN/DISPLAY.
Hapa tunaangalia Kioo pale ambapo kinakutana na hitilafu/kuvunjika kutokana na sababu mbalimbali, kwa leo tutazungumzia SABABU ambazo tumekuwa tukikumbana nazo na kwa jinsi gani ya ukiziepuka ili kutunza kioo cha Kompyuta yako. Kuweka
- Kompyuta/laptop kwenye begi pamoja na vitu vingine kama vitabu, madaftari au vitu vingine vigumu ambavyo vinaweza kuwa kisababishi kikubwa cha kuvunjika kioo. (ii) Kukalia begi/mfuko ambao umebeba Kompyuta/laptop yako, hapa utakuta mtu anakalia hilo begi bila kujua kitendo ambacho hupelekea kuvunjika kwa kioo. (iii) Pia kuna tabia ambapo unakuta mtu amepanda daladala hasa wanafunzi na kukuta gari imejaa na kusimama ndipo huchukua begi yake iliyobeba laptop/Kompyuta na kuweka kwenye “Staff Carier” kitendo ambacho ni hatari kwa Kompyuta yako. (iv) Mchanganyiko wa vitu vigumu sehemu moja mfano kwenye gunia, boksi pia huweza kusababisha kioo kuvunjika. Tatizo la kuvunjika kwa kioo linapotokea hakuna mbadala wa kuweza kuki “repair” bali ni kubadilisha kabisa hicho kioo na kuweka kingine. Dalili za kuvunjika KIOO; (i) Mstari mrefu unaoonesha kuvunjika kwa kioo unaotoka juu kuelekea chini. (ii) Kushindwa kusoma maandishi kwenye kioo (iii) Mwonekano mbaya wa maandishi kwenye kioo/screen ya Kompyuta yako. (iv) Rangi nyeupe kwenye kioo/screen huku kukiwa hakuna maandishi yoyote kwenye kioo (v) Rangi ya bluu kwenye kioo/screen (vi) Kioo kilichovunjikavunjika huku kukiwa na vitobo vidogo huku vikiongezeka kila iitwapo leo. Mambo ya kuzingatia pale unapoona dalili hizo ili uweze kubadilisha hicho kioo; Hapa ni kuangalia “MODEL NUMBER” ya Kompyuta yako hili kutambua Ukubwa/size ya kioo chako ambacho unataka kuweka kwenye Kompyuta yako. Tumekuwa tukikumbana na tatizo, watu wanashindwa kutofautisha kati ya aina ya Kompyuta na “Model number” kwa upande wa aina tunazungumzia mfano Dell, Lenovo, Hp, Accer n.k. Lakini ukizungumzia “Model number” hapa tunazungumzia kama HP Pavilion 14-B003TX C0P30PA, Dell Inspiron 14 3000 n.k. Kwa kawaida ukubwa/size wa kioo/sreen/display huwa ni inch 14, inch, 14, inch 17 N.B Vioo vya Kompyuta huingiliana, hapa tuna maana kioo cha Dell unaweza kukiweka kwenye HP, Accer, au Lenovo na kikafanya kazi vizuri, bali kinachoangaliwa sana sana ni Ukubwa/Size ya kioo chako. Somo litaendelea la Matatizo yanayoikumba Kompyuta yako na Suluhisho lake endelea kutufuatilia………… Karibuni sana kwa maoni na Ushauri, pia uwapo na tatizo usisite kunitafta
Comments
Post a Comment