Method Mwanjali beki wa Simba SC akanidhiwa kitambaa cha unahodha mkuu wa Simba SC akisaidiwa na Mohamedi Hussein ' Zimbwe jr ' . Hii ina maana rasmi Jonasi Mkude amevuliwa kitambaa hicho na atabaki chini ya uongozi huo mpya . Kwa zaidi misimu mitatu Jonasi Mkude alikuwa nahodha wa klabu hiyo . Bado hazijaelezwa kwa kina sababu za mabadiliko hayo ingawa taarifa za awali zinasema ni mabadiliko ya kawaida.
FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI
*Zijue faida za kula vyakula vyenye vitamin C.* Kuna aina nyingi za vitamini na zote zina kazi mbalimbali katika miili yetu. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwepo kwa vitamini nyingine nyingi ambazo bado hatujazivumbua lakini ni muhimu kwa afya zetu. Tutaendele kuzitafuta kadri tutakavyo wezeshwa. Kabla ya kukufahamisha vyakula vitupatiavyo vitaminC ni vyema nikakujulisha angalau faida chache tuzipatazo kwa kuwa na vitamini C mwilini. Vitamini C husaidia mwili kutumia madini ya(Kalsiamu) chokaa na virutubisho vingine kujenga mifupa na mishipa ya damu. Bila ya kuwepo vitamini C inakuwa vigumu kwa mwili kutengeneza mifupa na mirija ya damu. Hii huwathiri sana watoto wadogo na hata walio matumboni (mimba) ambao hasa mifupa yao bado inakuwa. Uimara wa meno pia hupungua kwa kukosekana calcimu inayotumika kwa msaada wa vitamini C. Vilevile vitamini C husaidia mwili kufyonza madini ya chuma kutoka kwenye vyakula. Kuna vyakula vingine ambavyo vina madini ya chuma ambayo bila msaada wa...
Comments
Post a Comment