Taifa Stars 'shughulini' na Amavubi, Mwanza

| SOKA
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo inashuka dimbani katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwakabili Amavubi (Timu ya taifa ya Rwanda) katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN.
Tayari kikosi cha Stars kipo jijini humo tangu Jumatano wiki hii kikijiandaa kwa mchezo huo, ambapo kocha mkuu Salum Mayanga amewakikishia watanzania kuwa wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya ushindi kwenye mchezo wa leo.
Kikosi cha leo kitamkosa beki Abdi Banda ambaye amepata dili ya kukipiga nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wa Rwanda, Kocha wake Mjerumani Antoine Hey amepeleka lawama zake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuupeleka mchezo huo Jijini Mwanza badala ya Dar es Salaam hali ambayo imewasabishia usumbufu mkubwa katika usafiri.
Pia kocha huyo ameeleza kushangazwa na kitendo cha uwanja huo wa Kirumba kufanyiwa ukarabati katika siku ambayo kikosi chake kilitakiwa kufanya mazoezi na kwamba anasikitishwa na hatua ya TFF kukataa kuusogeza mbele mchezo huo.
Mara ya mwisho Rwanda kucheza dhidi ya Tanzania ilikuwa katika michuano ya CECAFA mwaka 2015 nchini Ethiopia ambapo Amavubi ina kumbukumbu ya kupoteza kwa magoli 2-1 katika hatua ya makundi.
Mshindi kati ya Rwanda na Tanzania atacheza na mshindi kati ya Uganda na Sudan Kusini kwenye mchezo wa raundi ya tatu na ya mwisho ya mchujo mwezi ujao.
Kumbuka mchezo huu utakuwa LIVE kupitia ZBC 2 ambayo inapatikana kwenye king'amuzi cha Azam

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI

VYAKULA NA MATUNDA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

MATATIZO SUGU YA KOMPYUTA ,MBINU ZA KUONDOA TATIZO