MSUVA NA FARID MUSSA WATISHA

Msuva na Farid Mussa si wa mchezo mchezo 3rd August 2017 Mshambuliaji wa Kitanzania,Simon Msuva wa Difaa El-Jadida na Farid Mussa wa CD Tenerifa wameziongoza timu zao kupata sare katika michezo ya kirafiki iliyochezwa usiku wa kuamkia leo. Katika michezo hiyo ilishudia Difaa El-Jadida ikilazimisha sare 1-1 naYoussoufia Berrechid nchini Morocco wakati Hispania CD Tenerifa ilipata sare 2-2 na Las Palmas. Msuva akicheza mechi yake ya pili tangu alipotua Morocco alisababisha penalti iliyoanza bao la El Jadida kabla ya Youssoufia Berrechid kusawazisha. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga akizungumza baada ya mechi hiyo alisema ni jambo la furaha kwake kuzoea mazingira ya timu hiyo haraka tofauti na ilivyotegemewa. "Wananishangaa maana nimezoea haraka mazingira, mpaka sasa hakuna wakati mgumu ninao upata kutokana na mazingira yao namna yalivyo. "Huwa nafurahia sana, wanavyopenda kuwa karibu na mimi nadhani hawataki kuniona nikiwa mpweke," alisema Msuva. Naye winga wa CD Tenerife, Farid Mussa baada ya kuisaidia timu yake kupata sare 2-2 na Las Palmas katika mchezo huo wa kirafiki Alituma picha yake katika mtandao wake wa Instagram akiweka saini yake kwa mashabiki wake. Tangu kuanza kwa msimu huu wa maandalizi Farid ameanza kuonyesha kiwango cha juu katika harakati zake za kusaka kupata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa akitokea katika kikosi cha vijana alipokuwa msimu uliopita. Kwa hisani ya Mwanaspoti

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI

VYAKULA NA MATUNDA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

MATATIZO SUGU YA KOMPYUTA ,MBINU ZA KUONDOA TATIZO