"Ni kweli Kushinda ni furaha lakini sio hoja. Hoja ni
Kuwa na nia ya kushinda, Kutokata tamaa,
Kutokubali kushindwa pamoja na kuacha kutosheka na mafanikio uliyonayo"
George Lwandamina
FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI
*Zijue faida za kula vyakula vyenye vitamin C.* Kuna aina nyingi za vitamini na zote zina kazi mbalimbali katika miili yetu. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwepo kwa vitamini nyingine nyingi ambazo bado hatujazivumbua lakini ni muhimu kwa afya zetu. Tutaendele kuzitafuta kadri tutakavyo wezeshwa. Kabla ya kukufahamisha vyakula vitupatiavyo vitaminC ni vyema nikakujulisha angalau faida chache tuzipatazo kwa kuwa na vitamini C mwilini. Vitamini C husaidia mwili kutumia madini ya(Kalsiamu) chokaa na virutubisho vingine kujenga mifupa na mishipa ya damu. Bila ya kuwepo vitamini C inakuwa vigumu kwa mwili kutengeneza mifupa na mirija ya damu. Hii huwathiri sana watoto wadogo na hata walio matumboni (mimba) ambao hasa mifupa yao bado inakuwa. Uimara wa meno pia hupungua kwa kukosekana calcimu inayotumika kwa msaada wa vitamini C. Vilevile vitamini C husaidia mwili kufyonza madini ya chuma kutoka kwenye vyakula. Kuna vyakula vingine ambavyo vina madini ya chuma ambayo bila msaada wa...
Comments
Post a Comment