Yanga yaitungua Singida United 3-2 5th August 2017 Licha ya kutawala mchezo kwa sehemu kubwa, Singida United imeangukia pua baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Yanga kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Taifa. Singida United iliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata mkwaju wa penati kwenye dakika ya kwanza tu. Hata hivyo walikosa penati hiyo. Thabani Kamusoko akaifungia Yanga kwenye dakika ya tano kwa mpira wa adhabu baada ya Ibrahim Ajib kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18. Singida United ilisawazisha dakika tatu baadae kupitia kwa Usengimana. United iliyokuwa 'On Fire' ikafunga bao la pili kwnye dakika ya 23 kupitia kwa Simbarashehe aliyevunja mtego wa kuotea. Lwandamina alibadili kikosi chake chote kwenye kipindi cha pili na Yanga kufanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 83 kupitia mkwaju wa penati wa Amissi Tambwe. Emanuel Martini akaifungia Yanga bao ta tatu kwenye dakika za majeruhi. Matokeo hayo yaliibua nderemo kwa mashabiki wa Yanga huku wale wa Simba waliofurika uwanja wa Taifa kuishangilia Singida United wakitoka vichwa chini.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI

VYAKULA NA MATUNDA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

MATATIZO SUGU YA KOMPYUTA ,MBINU ZA KUONDOA TATIZO