utafiti wasema viazi vya kukaangwa vinachangia maradhi ya kisukari kwa wanawake wajawazito
Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani.
Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema.
mwanamke mjamzitoHaki miliki ya pichaPA
Image caption
Wanawake wajawazito watakiwa kupunguza ulaji wa viazi vya kukaangwa(chips) kuepuka ugonjwa wa kisukari
Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000.
Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga
Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari.
MbogaHaki miliki ya pichaAP
Image caption
Ulaji wa mboga mboga nyingine unaweza kuzuia hatari ya kisukari
Kubadilisha ulaji huu wa viazi (chips) kwa wiki kwa kula mboga mboga nyingine kunaweza kuzuia hatari hii, wanaeleza waandishi wa utafiti huu.
Wataalam wa masuala ya lishe nchini Uingereza wanasema vyakula vyenye wanga ama vya kuongeza nguvu na joto mwilini kama vile viazi, vinapaswa kuwa theluthi moja ya vyakula vinavyoliwa na watu.
Utafiti huo unatarajia kuchunguza nini chanzo cha maradhi ya kisukari yanayowapata baadhi ya wanawake wawapo wajawazito .
Utafiti huu umefuatia wauguzi wawili waliopata ujauzito kati ya mwaka 1991 na 2001. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuwa na maradhi ya kudumu kabla yaujauzitoo
FAIDA ZA VITAMIN C MWILINI
*Zijue faida za kula vyakula vyenye vitamin C.* Kuna aina nyingi za vitamini na zote zina kazi mbalimbali katika miili yetu. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwepo kwa vitamini nyingine nyingi ambazo bado hatujazivumbua lakini ni muhimu kwa afya zetu. Tutaendele kuzitafuta kadri tutakavyo wezeshwa. Kabla ya kukufahamisha vyakula vitupatiavyo vitaminC ni vyema nikakujulisha angalau faida chache tuzipatazo kwa kuwa na vitamini C mwilini. Vitamini C husaidia mwili kutumia madini ya(Kalsiamu) chokaa na virutubisho vingine kujenga mifupa na mishipa ya damu. Bila ya kuwepo vitamini C inakuwa vigumu kwa mwili kutengeneza mifupa na mirija ya damu. Hii huwathiri sana watoto wadogo na hata walio matumboni (mimba) ambao hasa mifupa yao bado inakuwa. Uimara wa meno pia hupungua kwa kukosekana calcimu inayotumika kwa msaada wa vitamini C. Vilevile vitamini C husaidia mwili kufyonza madini ya chuma kutoka kwenye vyakula. Kuna vyakula vingine ambavyo vina madini ya chuma ambayo bila msaada wa...
Comments
Post a Comment