utafiti wasema viazi vya kukaangwa vinachangia maradhi ya kisukari kwa wanawake wajawazito Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani. Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema. mwanamke mjamzitoHaki miliki ya pichaPA Image caption Wanawake wajawazito watakiwa kupunguza ulaji wa viazi vya kukaangwa(chips) kuepuka ugonjwa wa kisukari Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000. Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari. MbogaHaki miliki ya pichaAP Image caption Ulaji wa ...